@afmradiotz: Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limeendelea na oparesheni maalum ya ukaguzi wa vyombo vya moto barabarani kwa lengo la kuhakikisha usalama wa abiria na watumiaji wengine wa barabara katika Jiji la Dodoma. Oparesheni hiyo imefanyika leo chini ya uongozi wa Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, SSP Yussuf Kamotta, ambapo Jeshi hilo limefanikiwa kufika katika kituo cha mabasi ya mikoani kilichopo Nane Nane na kufanya ukaguzi wa kina kwa magari ya abiria. Katika oparesheni hiyo, Jeshi la Polisi limefanikiwa kulikamata basi moja la abiria ambalo lilikuwa na mizigo mingi ndani ya gari hilo kiasi cha kuhatarisha maisha na usalama wa abiria. Aidha, Jeshi la Polisi limeendelea na utaratibu wa kulichukulia hatua za kisheria dhidi ya dereva wa basi hilo. ✍️ @omari_koge #10YearsOfAFM #Miaka10YaAFM #VibesKubwaTOFAUTI