@shedy_quotes: “Nataka tu kukufanya uwe na furaha kuliko wakati wowote ule. Nataka ujihisi salama, kupendwa na kufarijiwa. Nataka ujue kuwa unaweza kunihitaji wakati wowote utakapokua haupo sawa, wakati macho yako yamejaa machozi, nami nitakukumbatia hadi ujihisi afadhali kidogo. Niko hapa kwa ajili yako kila wakati. Nakupenda ukiwa katika hali yako nzuri na hata ukiwa katika hali mbaya. Hakuna kitakachobadilisha hilo.” Penzi langu kwako si la kawaida, ni la kipekee penzi ambalo halielezeki kwa maneno ya kawaida. Wewe ni zaidi ya dunia yangu, wewe ni kila kitu kwangu. Nitabaki hapa, nitasalia kwa ajili yako, siendi kokote. Hata ndoto zangu haziwezi kunipeleka mahali pengine zaidi ya kwenye mikono yako. Wewe ni sehemu yangu ya usalama, sehemu yangu ya amani, na jina lako limeandikwa kwenye moyo wangu kwa herufi za upendo usioisha. “Nataka ujue kwamba ninaposema niko tayari kufanya chochote kwa ajili yako, ninamaanisha kabisa. Nitafanya kila kitu. Nakupenda sasa, na nitakupenda milele. Kila kitu kitakuwa sawa. Sisi tutakuwa sawa. Hii itadumu maadamu tunapendana na kuendelea kupendana siku zote za maisha yetu yote.” 🕊️ Nikupende leo, kesho, na milele… Kwa sababu wewe ni sehemu bora zaidi ya nafsi yangu. 🕊️ #tiktoktanzania🇹🇿 #MahabaMazito #UjumbeWaMoyo #ShedyQuotes
shedy_.🍀
Region: TZ
Monday 21 July 2025 18:32:31 GMT
Music
Download
Comments
ness :
💝
2025-07-28 20:05:41
1
P.E Shahdadi :
@Shekhe Bojo
2025-07-22 20:22:46
2
Gee veer :
@sua_finest
2025-07-22 09:57:58
2
To see more videos from user @shedy_quotes, please go to the Tikwm
homepage.