@nurul_kitab_wa_sunnah: Jiepushe Na Shaka, Kwani Halaal Na Haraam Imebainishwa, Moyo Ni Mfalme Wa Viungo Imepokelewa kutoka kwa An-Nu’maan bin Bashiyr (رضي الله عنهما) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: Hakika halaal iko wazi na haraam iko wazi. Baina ya mawili hayo kuna yenye kutia shaka. Wengi miongoni mwa watu hawayajui. Basi atakayejiepusha na yenye kutia shaka, atakuwa amejiepushia shaka katika Dini yake na heshima yake. Na Atakayetumbukia katika yenye kutia shaka, ataingia kwenye HARAAM. Kama mchunga anayechunga kando ya mipaka, ni haraka kulisha katika mpaka wa watu wengine. Zindukeni! Kila mfalme ana mipaka yake. Zindukeni! Kwa yakini mipaka ya Allaah ni HARAAM Alizoziharamisha. Zindukeni! Kwa yakini katika mwili mna kinofu cha nyama, kinapokuwa sahihi, mwili wote unakuwa sahihi. Kinapoharibika, mwili wote unaharibika. Zindukeni! Kinofu hicho ni moyo. [Al-Bukhaariy na Muslim] #islam #hadith #halal #haram #epuka\_shaka #imani #moyo #moyo\_ni\_mfalme #taqwa #uchamungu #uadilifu #uzuri\_wa\_dini #heshima #hidaya #uchaji\_mungu #njia\_sahihi #sunna #salaf #elimu\_ya\_dini #maarifa #msimamo #uaminifu #kujilinda #mwongozo #ukweli #maisha\_ya\_muislamu #usafi\_wa\_moyo #mafunzo\_ya\_mtume #muongozo\_wa\_quran

Nurul Kitab Wa Sunnah
Nurul Kitab Wa Sunnah
Open In TikTok:
Region: TZ
Sunday 17 August 2025 06:02:23 GMT
3941
316
9
33

Music

Download

Comments

abubakarramadhan47
abubakarramadhan47 :
Jazzakallah khayran
2025-08-17 10:59:16
1
sabrinamsomi
umm munira :
shukran ,,Allah akuhifadhi
2025-09-01 09:51:12
0
bigi.ba2
bigi ba :
❤❤❤
2025-08-17 12:13:47
1
aridjabili
Losembe :
🥰🥰🥰
2025-08-17 08:52:19
1
khalfan.seif.saleh1
KHALFAN SEIF SALEH :
♥️♥️♥️
2025-08-17 07:08:48
1
To see more videos from user @nurul_kitab_wa_sunnah, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About