@dr_waziri_health: Replying to @willuam60 Folic acid ni kirutubisho cha lazima kwa mama anayetaka au aliye tayari mjamzito. Wataalam wanashauri mwanamke aanze kutumia folic acid angalau mwezi mmoja kabla ya kushika mimba na aendelee nayo katika miezi ya kwanza mitatu ya ujauzito. Hii ni kwa sababu mshipa wa fahamu wa mtoto (neural tube) huanza kutengenezwa mapema sana, mara nyingi kabla hata ya mama kujua kuwa ni mjamzito. Dozi ya kawaida ni 400 micrograms (mcg) kila siku kwa mwanamke mwenye afya njema. Ikiwa mama ana historia ya matatizo ya mtoto kuzaliwa na dosari za uti wa mgongo (mfano spina bifida), ana kisukari, au anatumia dawa fulani, daktari anaweza kupendekeza dozi kubwa zaidi (kama 5mg). 👉 Kwa hiyo, kama tayari umeshapata ujauzito na hujaanza, anzisha mara moja na endelea angalau mpaka mwezi wa 3 wa ujauzito (miezi mingine pia unaweza kuendelea kwani pia husaidia damu na ukuaji wa mtoto). Follow kwa Elimu zaidi. #ticktocktanzania🇹🇿 #followersthankyou🥰 #creatorsearchinsights #trendingvideo #ticktockzanzibar💜

DR_WAZIRI
DR_WAZIRI
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 21 August 2025 10:44:04 GMT
88304
920
31
81

Music

Download

Comments

habswety604162
cute girl :
Mimi nina miez miwili naingia wa3 sijaanza clinic wala kutumia folic asid jeee ni Salam kwangu
2025-08-23 09:35:41
2
brilliant4726
Brilliant :
Dr mimi ujauzito wangu ni wk 11 nikaenda kuanza clinic nikapewa Folic Acid nimemeza kimoja ucku asubuhi damu zinatoka je huwa zinamadhara
2025-09-22 12:09:36
1
stella.peter60
...♥️ :
je ukianz kutumia n miez minne kasoro Kuna shida?
2025-08-21 19:02:17
4
faida.makame
Faida Makame❤️ :
doctor mimi ni mjamzito wa wiki mbili naweza kutumia folic avid
2025-09-24 14:20:11
3
jacklinecharles273
jackline :
mi ninamiez 7 xijatumia
2025-09-08 04:55:24
3
saskaycute245
it's -A-aliyah 💞💞💞 :
lkn si naskia papaya si nzuri kwa mja mzito@
2025-09-10 14:40:35
1
safinalioche509
serphiner :
folic asid n mzur kwa afyaa ya mwanao ndy maana pale unapojihisi mjamzito unatakiwa kuanza klinik na kuanza kutumia folic acid kumkinga mtoto magonjwa
2025-09-02 10:42:02
1
jenshayo
ma.twins :
na kama Nina dam nyingi had nashikwa kizunguzungu,mimba Iko 9 weaks nifanyeje coz nateseka sana
2025-08-31 14:45:57
2
asha.juma155
Asha juma :
samahani doctor nizip hizo foric asd au tunazopewa kiriniki
2025-10-14 07:45:15
0
raybcute8
raybcute :
Dr me nilianza clinic na miezi 2 wakanipa folic acid za aina2 na kunywa mchana 2 na usiku kabla ya kulala aina nyingine ile ya fefo kimoja ni sawa kweli
2025-10-01 15:18:59
2
user6085846546195
wemaely :
kwa kawaida unatakiwa kutumia miez 3 kabla ya kubeba ujauzito ila kuna wale ambao unajikuta teari wewe ni mjamzito unaanza siku hiyo ulojua
2025-10-01 04:43:08
1
shamimadam695
Shamim Adam695 :
dokta habar iv kutokuwa na mstar wa mimba kwa mjamzito ni kawaida maana mimba zangu miez mi 3 tu unatoka ila hii miez mi5 lakin hakuna
2025-09-17 07:19:26
1
sarahmotto343
official.sara.. :
mimi ndio sieleweki natumia nilijisikia kumeza ila mara nyingi huwa simezi
2025-09-14 20:13:25
1
user6181120715933
mzambuli :
folic acid ni nn
2025-10-04 09:57:24
1
innocent.daniel3
p wa j :
Habali dr mimi nina mimba ya wek mbili ninatumia hii Folic Acid ila sasa naona damu kdg kdg inatoka kuanzia tareh 28 mpk tareh 30 yaan jana ila kuna vidonge vya rangi ya pinki navitumia namshukuru MUNGU leo toka asubuhi sijaona damu sasa sijajua kuwa ni folic Acid inasababisha hii hali?
2025-10-02 10:50:38
2
safinalioche509
serphiner :
inamkinga na magonjwa kam mgongo wazi, mdomo wazi na kichwa kikubwaa kwa mtoto
2025-09-02 10:42:39
3
officiallymrsramadhan
Officialmrsramadhan :
Mimi nina mwezi na nimesahau za kutumia folic acid je nipo sahihi
2025-09-03 10:58:40
0
To see more videos from user @dr_waziri_health, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About