@rfi_sw: Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mpango wa mchakato wa amani ya kitaifa na jumuishi umewasilishwa jana (Jumatatu) mjini Kinshasa. Kwa miezi kadhaa, mpango huu wa mazungumzo ya kitaifa umeongozwa na makanisa ya Kikatoliki na Kiprotestanti (CENCO na ECC) kabla ya hapo jana kuunganishwa na madhehebu yote ya dini. Mpango huu wa upatanishi ambao unajumuisha wadau wote ikiwa ni wa kisiasa, kijeshi na kijamii, unalenga, kusaidia kumaliza mzozo wa kisiasa na usalama unaoikabili DRC, wakati uasi wa AFC/M23 unadhibiti maeneo makubwa ya eneo la mashariki mwa nchi. Kwa sasa, viongozi wa kidini wanasubiri tu tangazo rasmi la kuanza kwa mazungumzo hayo na kuomba wadau wa kimataifa kusaidia kufanikisha mpango huo. #fyp #rdc #cenco #M23 #ECC #FelixThisekedi