@mecamedia123: 🇹🇿 Shule zote kufungwa katika kambi za wakimbizi Nyarugusu na Nduta – Serikali yashinikiza wakimbizi wa Burundi kurejea nyumbani Serikali ya Tanzania, kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), imetangaza kufungwa kwa shule zote za Msingi na Sekondari katika kambi za wakimbizi za Nyarugusu na Nduta. Uamuzi huu unalenga kuharakisha mpango wa kuwarejesha wakimbizi wa Burundi nchini kwao kufikia Juni 2026, kufuatia tathmini inayodai kuwa hali ya usalama na amani imeimarika nchini Burundi. Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na MecaMedia Africa, zaidi ya wakimbizi 100,000 wanatarajiwa kufutiwa hadhi ya ukimbizi ikiwa hawatakubali kurejea kwa hiari kabla ya muda uliowekwa. Serikali imesisitiza kuwa hatua hii ni sehemu ya mpango wa kurejesha wakimbizi kwa heshima na usalama, huku ikiahidi msaada wa kimataifa katika mchakato huo. Hata hivyo, baadhi ya mashirika ya haki za binadamu yameelezea wasiwasi kuhusu mustakabali wa elimu ya watoto wakimbizi, wakihimiza suluhu za kibinadamu zinazoendana na haki za msingi za binadamu. ✍️ Mwandishi: Mangwa – MecaMedia Africa 📖 Soma zaidi kwenye: www.mecamediaafrica.com #Tanzania #Burundi #Wakimbizi #Nyarugusu #Nduta
Mecamedia
Region: US
Saturday 18 October 2025 01:44:35 GMT
Music
Download
Comments
munyamwezi 💔 :
atutaki uhogo brother
2025-10-18 02:06:02
2
Kariakoo_brands :
hapana hiyo ni ukiukaji wa haki za binadamu
2025-10-18 10:57:11
3
Pâmella isaro 🇧🇮🇹🇿 :
Ni hâtali
2025-10-18 13:54:34
2
Etho wangu 😘❤️ :
acha uwongo wewe 🤣
2025-10-18 14:32:06
1
charles nico305 :
waondoke mapema kabisa
2025-10-18 16:50:21
1
Zabron Mshikana :
Uwongo
2025-10-18 17:08:41
1
KING :
nyango man congo
2025-10-20 05:16:19
0
mbaya iyo :
ndo sawa thx good 😊😂😂🤘
2025-10-20 11:36:33
0
OLIVIER KALOS :
pale Muna coma
2025-10-18 04:44:19
1
Furaha-Huruma :
achani roho mbaya
2025-10-20 10:50:35
1
Benedicte Mihigo :
hakuna amani, munaogopa vita ngapo zote
2025-10-18 04:40:20
1
mr: li mjj kajw ksm :
kama amani imerejea warudi kwao wakajenge nchi yao
2025-10-20 17:09:52
0
🌹mamy🌹❤️ :
wakuje kabisa 🥰🥰😂😂
2025-10-20 08:43:19
0
Mr Rich :
Tunataka haki yetu 😁
2025-10-19 18:28:03
0
ELPHAZ JAVAN AMON AMON :
wawaache hao ni wafrika
2025-10-19 06:15:58
1
mr maokoto 45 :
camanda siro yulee
2025-10-19 14:28:08
0
majaliwa 077 :
kwann mnawafukuza warundi embu waacheni
2025-10-19 12:44:54
1
jenny_jr4 :
@itsjuju40 @fedha_11 @Fifi🔐🤎 @Benjamin Lee (Old is gold)
2025-10-18 16:17:05
0
kaa mbali na mimi :
😁
2025-10-18 02:38:45
1
swagger_mama :
😅😅😅
2025-10-20 14:41:33
0
iranzi :
😳
2025-10-18 15:35:02
0
To see more videos from user @mecamedia123, please go to the Tikwm
homepage.