@mrsmiss00: Mimi ni baba umri wangu ni miaka 39, nimeoa na tumebarikiwa watoto watatu mpaka Sasa. Mimi ni mwanajeshi ila Kwa Sasa nimeacha kazi baada ya kupata matatizo ya kisukari iliyo pelekea Mimi nikakatwa mpaka mguu, ni mwaka wa pili Sasa toka nikatwe mguu lakini hali yangu bado ni mbaya sana na mara nyingi nalazwa sana hospital pia huu mguu ulio bakia uko kwenye hatari pia ya kukatwa. Dada kama ujuavyo watu wenye sukari huwa ni ngumu tena kufanya tendo la ndoa au hata ukifanya uwezo siyo ule ulio kuwa nao mwanzo, Mimi Kwa Sasa uwezo wa kufanya tendo haupo kabisa Kwa sababu Afya yangu ni mbaya sana, nateseka sana. Kilicho fanya nikutafute dada yangu ni mambo ambayo ananifanyia mke wangu, Kuna siku niliwahi kuona kwenye simu yake Wana wasiliana na mwanaume mwingine pale pale nikawa nimepata jibu kuwa mke wangu amesha pata mwanaume mwingine, niliumia sana, nikalia sana, ila Kwa vile Sina uwezo wa kumridhisha tena ikabidi tu nimuombe hayo mambo yake awe anafanyia mbali na siyo kwangu au kunionyesha wazi wazi, nikamuomba pia ahakikishe watoto wasijue hicho kitu. Dada, ilikuwa jumatano usiku nilisikia nyuma ya nyumba kishindo Cha mtu, ikabidi nichukue magongo yangu nikatoka taratibu mpaka nje, Kwa vile nyumba Ina ina uzio ikabidi nizunguke taratibu kuangalia nyuma, Kwa macho yangu nilimkuta mke wangu kakumbatiana na mwanaume huku mke wangu kavaa nguo ya ndani huku taulo lipo chini, yule mwanaume baada ya kuniona alinikimbilia nikajua anakuja kunipiga, alicho fanya ni kunisukuma nikandondoka chini akawa amekimbia, siku bahatika Kumuona sura, na mke wangu akawa amepitia upande wa pili akarudi ndani. Haya yote sijamuambia mtu yeyote nafikiria hata nifanye nini nashindwa, nawaza niwaambie ndugu zangu Ili wanisaidie kuachana na huyu mke wangu ila hofu yangu ni watoto bado wadogo na sipendi walelewe na mtu mwingine, nawapenda sana wanangu, najua maisha yangu hapa Duniani yame baki kidogo tu ila napenda niendelee kuwaona wanangu wakiwa na furaha. Ukweli dada yangu Kwa Sasa naona mke wangu ndiye anaye nitesa kuliko hata huu ugonjwa wenyewe nashindwa hata Cha kufanya, nateseka sana sioni sababu ya mimi kuletwa hapa Duniani mateso ni makali, sijamuelezea mtu yeyote kuhusu hii tabia ya mke wangu hata dada wa kazi nimemkataza asije kumuambia mtu yeyote lakini imebaki kama mateso kwangu.
STORI ZA KIBAO 📖
Region: TZ
Wednesday 17 December 2025 14:57:54 GMT
Music
Download
Comments
saida :
asante 😆😆mnakuwaga jeur sana mkiwa wazima kiafya mm wakwangu naomba apate ajali Ile mbaya
2025-12-18 07:54:26
51
maryam :
Allah akupe subra.....swali sana omba mungu atakusaidia....mitihn ndio sehemu ya maisha...bila mitihn huwezi kupata faraja mbele yake.....jikaze usikate tamaa mbele faraja ipo.....na umuombe mungu sna kizazi chako kisije kulannda hio tabia ya mama yao......
2025-12-18 03:53:21
34
Jackline Madeje :
safi pumbavu 😳😳
2026-02-04 09:41:48
0
kemmy shayo :
Hata ingekuwa ww ungefanya hivyohivyo
2026-01-17 06:56:08
1
Reymbucha♥️💕 :
pole sana lkn labda na ww ilikua ndo tabia yako
2025-12-19 04:21:37
13
Mama G :
yupo Sawa ungekua wew ungeoa kabisa atakuonea huruma ambaye hajapitia maumivu yenu
2026-01-17 18:26:48
8
user7619272904100 :
pole sana nitafute nikuonyeshe dawa ya kisukar mm nilikuwa muhanga ila nimepona kabisa
2026-01-02 20:01:26
8
shonie :
wema ni akiba nadhani na wewe ulimtesa sana.
2026-01-05 08:43:37
7
Adhiambo❤️ 🦋 :
Kwa vile ni mwanajeshi wacha likupate kwa niaba 😏
2026-01-17 09:27:19
5
pliampawe♥️ :
pole kaka,mtegemee Mungu,sana
2026-01-27 12:09:06
0
Husna Ismail :
pole sana
2026-02-10 08:08:37
0
user442216155211A Amuuni :
Pole sana kaka mungu akupe nguvu
2025-12-18 07:28:10
8
Jl Lau nobifu :
pole kk lakini muamini mungu kureta wanaume Wenda mungu atakujibu
2025-12-18 21:22:36
5
Mody Zombie :
kuna binadamu unaongea vibaya kama hii dunia niya kwenu
2025-12-18 17:33:40
7
mani :
sema alhamdulillah alafu muachie mungu
2026-02-08 05:44:24
1
cutee hellen :
pole kakaangu
2026-01-19 20:38:35
0
omushooraa :
🙏🙏🙏🙏pole sana amini mungu ndoo muamuzi wa hatima ze usiwaze kaka
2026-03-03 16:26:20
1
Rose Mary :
pole sana
2026-01-16 17:17:16
3
mwambie aende kwao Hilo tatizo kubwa atakusumbua
2026-01-19 16:34:43
3
Ngasala :
hooi pole
2026-01-19 16:06:17
1
Rahma Mwinyi :
shenzi sanaa huyo.mke😏😏😏😏😏
2025-12-18 06:36:40
3
Sofia Kazamaso :
polee sanq njoooo kwangu
2026-01-16 14:55:09
3
Raymond Joseph mipawa :
pole sana ndg yangu mungu akusaidie uwe na amani
2026-01-16 15:47:44
3
obby dady :
poleee mkuu mungu akutie nguvu tu
2026-02-15 12:42:48
1
To see more videos from user @mrsmiss00, please go to the Tikwm
homepage.